dc.description.abstract |
Mabaḍiliko ya kisemantiki ni haliya isiyopingika katika ukuwaji wa luǧa
yoyoṭʰe ulimwenguni. Pahala pamoja ambapo maneno huhifaďiwa k̇ a
matumiyaji ya sasa na ya vizazi vijavo ni makamusini. Makamusi
hukusanya maana za mingi ya maneno yanayotumika katika jamii na k̇ amo
mabaḍiliko ya kisemantiki hujiṭokeza. Makala haya yamelenga kuṭaťmini
maana ya neno “hongera” k̇ enye makamusi ya kiSwahili ya awali na ya
kileo minṭarafu ya uṭamaḍuni wa waSwahili, wekahazina wa luǧa ya
kiSwahili. Maďumuni ya uṭafiṭi wetu yalikuwa kučanganuwa maana ya
neno hongera kama msamiyaṭi k̇ enye makamusi; kučunguza maana ya neno
hongera katika mila za waSwahili; na kuṭaťmini uwafiki wa matumiyaji
mapana ya neno hongera katika jamii leo. Naďariya ya Usemezano,
iliyoongoza uṭafiṭi huu, inafafanuwa kuwa maana haswa ya neno
hupatikana k̇ a k̇ angaliya vigezo va usuli, mapisi, mukṭaďa, sajili,
uṭamaḍuni, ainaṭi za luǧa zilizomo k̇ enye lugha hiyo; la sivo, tuṭapata
maana ya kijuujuu au ya kikamusi. Data yetu tuliikusanya k̇ a kuwauliza,
kupitiya mahojiyano yasomuunro, wasailiwa 5 wa marika zetu (wa miyaka
55 k̇ enra chini) na piya wazee 5 (wa miyaka 70 na zaiḍi) kuhusu usuli,
mukṭaďa wa matumiyaji, na mafafanuzi ya kiṭamaḍuni juu ya neno hilo
“hongera”. Aiďan maaṇḍiko ya waṭaalamu na makamusi yenye ťika piya
yalipitiwa na kučanganuliwa ili kutupa data ya neno “hongera”; kupunguza
mlemeyo wowoṭʰe wa wahijowa; na piya kuhakikiša mayelezo ya
wasailiwa. Uṭafiṭi wetu uliťibiṭiša kuwa hongera latumika k̇ a maana ya “kupongeza” ṭu k̇ enye makamusi ṭajika ya kiSwahili sanifu ya kileo, k̇ a mfano,
Kamusi Kuu ya Kiswahili (2016). Awali, katika makamusi asasi ya Krapf
(1882) na Sacleux (1891/1939), maana ya hongera imeťubuṭu kumaaniša
awamu katika šerehe ya ṭohara au ni kufariji k̇ a mikasa iliyompata mtʰu.
Aiďan, maṭokeyo yetu yaligunruwa kuwa “hongera” ni neno limaanišalo
“pʰole” katika kiSwahili Asiliya (lahaja za ṗani Afrika Mašariki) lakini
maana hii imevunjwa na maana ya kiṭamaḍuni k̇ a sababu ni awamu katika
šerehe ya ṭohara, piya ni awamu katika šerehe ya harusi ya kiSwahili
haswahaswa wakati wa ḃanaharusi k̇
ingiya nrani kuwonana na biharusi
kimwili. Kimila ya waSwahili neno hili ni ṁiko wa daraja ya juu—lahusu
ngono—hivo hwanika ungonočoro linapotumika pasipo. Lengo la uṭafiṭi
huu ni kušauri ifikiriwe ṭena maana ya neno hongera katika makamusi ya kileo. Uṭafiṭi huu una naṭija k̇ a wanaleksikografiya kufanya uṭafiṭi zaiḍi
wanapotengeza makamusi. Piya uṭawafaa wanaiḍara ya uṭamaḍuni katika
mamlaka kujuwa asili na mila za watumiyaji wa luǧa hii ya kiSwahili na
nyenginezo ṇčini. |
en_US |