dc.contributor.author |
Muigai, Mary Njambi |
|
dc.contributor.author |
Mwamzandi, Issa |
|
dc.contributor.author |
Oduori, Robert |
|
dc.date.accessioned |
2024-08-19T06:55:03Z |
|
dc.date.available |
2024-08-19T06:55:03Z |
|
dc.date.issued |
2024 |
|
dc.identifier.citation |
Muigai, M. N., Mwamzandi, I., & Oduori, R. (2024). Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za SA Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010). Journal of Kiswahili and Other African Languages, 2(1), 10-19. |
en_US |
dc.identifier.issn |
2958-4914 |
|
dc.identifier.uri |
http://ir-library.kabianga.ac.ke/handle/123456789/867 |
|
dc.description |
Jarida la Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A.
Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010) |
en_US |
dc.description.abstract |
Makala haya yanachunguza matumizi ya uchopekaji wa
vipande vya simulizi katika riwaya mbili za S. A. Mohamed,
Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010). Uchunguzi huu
uliongozwa na Nadharia ya Ubaadausasa ambayo
hupendekeza uanuwai wa mawazo kwa kukaidi kuwepo na
mtazamo mmoja wa kueleza ulimwengu na tajriba za
binadamu, au simulizi kuu. Uchanganuzi umedhihirisha kuwa
mwandishi wa riwaya hizi alitumia kimakusudi vipengele vya
kibaadausasa ili kukaidi simulizi kuu zilizotawala. Riwaya hizi
zilitumia uchopekaji wa vipande vya simulizi kuvuruga
urazini, mshikamano, na muumano wa usimulizi wa riwaya za
kimapokeo. Kimaudhui, riwaya hizi zinasaili mwelekeo chanya
uliohusishwa na uhuru. Zinaonyesha kuwa mataifa mengi ya
Afrika yametawaliwa na hali ya utamauishi baada ya uhuru.
Vilevile, misaada inayotolewa na mataifa ya ulaya hutumika
kama chambo cha kueneza ukoloni mamboleo katika mataifa ya
Afrika. Hali kadhalika, riwaya hizi zinaonyesha changamoto
ambazo wahamiaji hupitia wanapohamia ughaibuni kutafuta
maisha bora. Ni bayana kuwa mwandishi wa riwaya hizi
ametumia mtindo wa uandishi wa ubaadausasa kama mbinu ya
kiumbuji inayokaidi uandishi wa kimapokeo. Vilevile, riwaya
hizi zimetumika kudhihirisha fujo, ghasia, na ukosefu wa
mshikamano katika ulimwengu wa karne ya ishirini na moja. |
en_US |
dc.language.iso |
en |
en_US |
dc.publisher |
Journal of Kiswahili and Other African Languages |
en_US |
dc.subject |
Simulizi kuu |
en_US |
dc.subject |
Uanuwai |
en_US |
dc.subject |
Ubaadausasa |
en_US |
dc.subject |
Uchopekaji |
en_US |
dc.title |
Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010) |
en_US |
dc.type |
Article |
en_US |