Abstract:
Makala haya yalichunguza jinsi wasanii wa vitabu vya fasihi ya watoto wamefuma tashbihikatika kazi zao ili kueleza maudhui yanayowalenga watoto kwa kuongozwa na nadharia ya umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure (1916). Kupitia kwa njia ya kiupekuzi na uchanganuzi matini, vitabu vya Kisasi Hapana, Nimefufuka, Sitaki Iwe Siri, na Wema wa Mwanaviliteuliwa kimakusudi, vikasomwa na kuchanganuliwa. Tashbihi mbalimbali na maudhui ya familia, elimu, nidhamu, bidii, ugonjwa na kifo yalitambuliwa na kujadiliwa kwa undani. Uhusiano kati ya tashbihi na maudhui hayo ulidhihirishwa. Matokeo ya jinsi tashbihi zinavyofanikisha kueleza maudhui yaliwasilishwa kithamano. Utafiti huu umeonyesha tashbihi na maudhui katika kazi tulizohakiki na pia unachochea washikadau katika uwanda wa fasihi ya watoto kuhakiki kazi za watoto kablakuwateulia kuzisoma.