Abstract:
Katika masiku ya hivi karibuni mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali nchini Kenya yamezinruka na kuonya kuhusu barabara wanasiyasa wanayot̪aka kutupeleka huku wakivutiya mikao yao katika Uchaguzi Mkuu unaokuja baad̪ a ya mud̪a kid̪ogo t̪u. Kwa vile kila mwamba ngoma huvutiya kwake, basi, ikawa kumsetʰa mwenziyo ni sawa. Mbiyu za mgambo zilipoanza kufikiriwa kulizwa, Serikali Kʰuu imekuja haraka na kwingiliya kati ili kuweka nidhamu isohat̪ arisha amani ya nchi. Hat̪uwa hii ya Serikali Kʰuu ni jambo la kupongezwa na kushukuriwa. Kama wasemavo wazee wetu wat̪ukufu waloitumikiya nchi hii kwa moyo wao wot̪ʰe, kura ni wingu la kupitʰa na keshowe kut̪akucha. Naswaha ya neno letu ni kwamba makunri yot̪ʰe yaangaliye twat̪oka wapi, tukoje hivi sasa, na kesho twait̪araji siku iwe njema vipi. Tukiyangaliya usawa wa binad̪amu kimaumbo yao, sisi twasema katika mwingiliyano wa lugha zao, piya, hakuna ilo bora kuliko nyengine. Lugha zilizomo Kenya ni nyingi na kila moja ina jukumu la kwenreleza ushikamano na ufungamano ili shabaha na lengo letu liwe moja: kuinuwa Kenya kihali na kimali. AMANI BAINA YA JAMII ZETU IMO KATIKA KILA KITʰU.