dc.contributor.author |
Kurgat, Ezekiel |
|
dc.date.accessioned |
2021-10-19T07:01:45Z |
|
dc.date.available |
2021-10-19T07:01:45Z |
|
dc.date.issued |
2019 |
|
dc.identifier.citation |
Kurgat, E., & Mwamzandi, I. (2019). Usemezano Katika Nyimbo za Amani: Athari za Muktadha wa Kijamii Katika Utunzi na Uimbaji wa Nyimbo za Mhubiri Joel Kimetto na Mwinjilisti Philip Rono. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 1(3), 118-128. |
en_US |
dc.identifier.uri |
http://ir-library.kabianga.ac.ke/handle/123456789/224 |
|
dc.description |
Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili wa sanaa katika Kiswahili katika chuo kikuu cha Kabianga |
en_US |
dc.description.abstract |
Utafiti huu ulichunguza usemezano katika nyimbo za amani za jamii tatu za Kenya. Nyimbo
zilizoshughulikiwa ni zile zilizoimbwa baada ya ghasia zilizoshuhudiwa nchini Kenya baada ya
uchaguzi wa kitaifa uliofanywa mwaka wa 2007. Kazi hii ilichochewa na uharibifu mkubwa wa
mali na vifo vya watu usioweza kumithilika hasa kwa vile nchi ya Kenya ilikuwa haijawahi
kuipitia hali kama hiyo wakati mwingine. Azma kuu ya utafiti huu ilikuwa kubainisha sifa za
usemezano katika nyimbo za amani miongoni mwa jamii za Wakipsigis, Wakisii na Waluo. Kwa
kufanya hivyo, uchunguzi huu ulilenga kuchunguza athari za mazingira na muktadha wa kijamii
katika utunzi na uimbaji wa nyimbo za amani. Aidha, kazi hii ilidhamiria kufafanua dhana ya
shani kama inavyojitokeza katika nyimbo za amani. Hali kadhalika, kazi hii ilibainisha nyimbo
kama kauli ambazo hujibu na kutarajia majibu kuhusu amani. Utafiti huu ulishughulikia jumla
ya nyimbo ishirini zenye maudhui ya kukuza amani na maridhiano kutoka jamii tatu za Kenya
zilizoathirika katika ghasia zilizozuka baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa. Jamii
zenyewe ni Wakipsigis, Wakisii na Waluo. Utafiti huu uliendelezwa katika Kaunti za Kericho,
Bomet, Nyamira na Nyando na ulishirikisha nyimbo zilizoimbwa baina ya mwaka wa 2008 na
2013. Nyimbo tano kutoka kila jamii husika ziliteuliwa kimakusudi na kisha kuhakikiwa.
Nyimbo nyingine tano zilizoimbwa kwa lugha ya Kiswahili kutoka jamii tatu teule katika
uchunguzi huu zilishughulikiwa pia katika kazi hii. Nyimbo za wanamuziki kutoka jamii
zilizohusishwa zilikusanywa na kuhakikiwa. Kwa hivyo, data za kimsingi zilitokana na nyimbo
zilizorekodiwa kwenye sidii. Aidha, uchunguzi maktabani uliendelezwa kwa kurejelea kazi
mbalimbali za awali zilizowahi kushughulikiwa kuhusu nyimbo. Habari nyingine zilikusanywa
katika mtandao. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya usemezano iliyoasisiwa na Mikhail
Bakhtin. Uchanganuzi wa kimaelezo ulitumiwa katika kuchanganua data. Matokeo ya utafiti
huu yanaonyesha kuwa nyimbo huwa na uwezo mkubwa wa kuielekeza jamii kwa njia
mbalimbali. Kwa sababu hii, jamii hupokea ushauri na maelekezo juu ya umuhimu wa kukuza
utangamano, amani na maridhiano kupitia nyimbo. Aidha, nyimbo huweza kutumiwa kama njia
mojawapo ya kuiponya jamii pindi inapokumbwa na hali tata iletwayo na michafuko. |
en_US |
dc.language.iso |
other |
en_US |
dc.publisher |
Jarida la Afrika mashariki la masomo ya Kiswahil |
en_US |
dc.subject |
Usemezano |
en_US |
dc.subject |
Nyimbo za amani |
en_US |
dc.subject |
Jamii |
en_US |
dc.title |
Usemezano katika nyimbo za amani miongoni mwa jamii tatu teule za Kenya |
en_US |
dc.type |
Thesis |
en_US |